Monday, July 24, 2017

HABARI NJEMA KWA WAKULIMA, NAFAKA BADO YASHIKILIA PALE PALE.

Hali ya soko masokoni katika masoko makuu ya mikoani hapa nchi bado iko vizuri, ambapo mazao hayajapanda wala kushuka kulinganisha na wiki iliyopita. Gunia la mchele la kilo 100 kwa soko la mkoani Morogoro (Mawenzi) limebaki kuwa 180,000tsh kwa bei ya chini na 180,000tsh kwa bei ya juu. Bonyeza hapa kupakua taarifa ya tarehe 10/07/2017 kuona bei ya nafaka ilivyokuwa sokoni.

Wednesday, July 12, 2017

BEI ZA MAZAO SOKONI ZASHUKA.

Mazao mbali mbali sokoni yameshuka bei kwa sasa kulinganisha na mwezi wa sita. Hii hutokana na mavuno kuwa mengi na kusababisha kushuka bei kwa mazao kama vile mahindi, mchele, viazi mviringo na mazao mengine katika masoko hapa nchini.

KILIMO CHA PILIPILI HOHO.

Kilimo Bora Cha Pilipili Hoho Na Faida Zake.

Utangulizi.
Pilipili   hoho ni moja ya mazao ya viungo ambalo hulimwa kwa wingi Mikoa  ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Mbeya  na Iringa.
Zao hili hutumika kama kiungo kwenye vyakula mbalimbali kama vile vyama, viazi na ndizi. Vilevile hutumika katika kutengeneza kachumbari na kuweza kukaushwa na kusagwa ili kupata unga.
Viini lishe vinavyopatikana katika pilipili tamu au hoho ni

KILIMO CHA TANGAWIZI.

KILIMO CHA TANGAWIZI.

Utangulizi.
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China.

Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi

KILIMO CHA MBAAZI.

JIFUNZE KILIMO CHA MBAAZI.

Utangulizi
          Mbaazi ni zao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa kama zao la biashara kutokana na kuwa na soko zuri la Mbaazi.Mbaazi ina kiasi kikubwa cha protini.Mbaazi inaweza kutoa mavuno ya tani 3.5 hadi 4 kwa hekta

HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI
            Mbaazi zinafaa kulimwa katika maeneo ya ukanda

KILIMO CHA UYOGA.

KILIMO CHA UYOGA

Utangulizi
Miaka ya karibuni, utaalamu wa kuotesha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, urahisi wa teknologia ya kuotesha katika mazingira ya Tanzania na soko lake kwa wananchi na katika hotel.

JINSI YA KUSINDIKA SOYA

Sindika soya ili kuongeza thamani na ubora wake

Soya ni zao mojawapo kwatika mazao ya jamii ya mikunde ambalo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mtwara,Ruvuma, Morogoro, Rukwa, Lindi,Mbeya, Iringa na Arusha. Zao hili huwa na virutubisho vingi kama vile wanga, protini, mafuta, madini na hata vitamini. Aidha, lina sifa ya kuwa na kiasi kikubwa cha protini kinachofikia hadi asilimia 40. Soya ni zao la muda mfupi ambalo

KUSINDIKA PILIPILI

USINDIKAJI WA PILIPILI KALI

Aina nyingi za pilipili kali (Chillies) hulimwa katika maeneo madogo katika sehemu nyingi nchini Tanzania na zao hili hulimwa kama zao la chakula na kibiashara.
Mavuno mengi ya zao la pilipili kali hupatikana kwa kuzingatia kanuni kama ifuatavyo;

Kuchagua aina ya mbegu
•  Chagua aina ya mbegu bora kulingana na mahitaji ya soko.
•  Chagua aina inayovumilia magonjwa, wadudu waharibifu na inayokomaa mapema.

Kuweka mbolea

KILIMO CHA MIGOMBA (NDIZI)

KILIMO CHA MIGOMBA (NDIZI)

Utangulizi
Niukweli usiopingika kuwa kilimo cha migomba(ndizi) hapa Tanzania kimekuwepo kwa miaka mingi sana iliyopita.Kilimo hichi kimejizolea umaarufu sana sababu zao la ndizi linalopatikana kwenye migomba limekuwa likitumiwa na jamii na sehemu kubwa ya inchi yetu kwa chakula.Baadhi ya mikoa inayolima

Tuesday, July 4, 2017

BEI YA MCHELE YABAKI PALE PALE KWENYE MASOKO.

Bei ya mchele imeonekana kutoshuka sokoni kulinganisha na mazao mengine. Mwezi wa sita tarehe 23 kwa soko la Buguruni (Ilala, Dar Es Salaam) gunia la 100kg lilikuwa linauzwa kati ya shilingi

Monday, July 3, 2017

KILIMO CHA TANGAWIZI

  • UTANGULIZI
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Ambao huonekana kama mizizi ya mmea. Mmea huu kitaalamu huitwa zingiber officinale.
       Asili ya mmea huu sehemu za kitropiki za bara la Asia hasa nchi za china za india. Zao hili huzalishwa kwa wingi nchini Jamaica.
    Hapa nchini zao hili huweza kustawi katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Ruvuma, kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.



  • MATUMIZI
Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na changamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, n.k
   Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k.

      
  • TABIA YA MMEA
Kama nilivyodokeza hapo juu, mmea huu huvunwa kama Tunguu hivyo basi; hutambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi.
       Ingawa hadi sasa kitaalamu haijasibitishwa kuwa ni aina gani ya tangawizi hulimwa hapa Madaba. Wengine husema ni white Africa (Jamaica)na wengine husema cochin (flint). Ambazo ndio maarufu hapa nchini Tanzania.
       Kikubwa sio aina ya mmea bali uwezekano wa kustawi na kutoa matunda mazuri, aina hizi hutofautiana tu katika majani na ukubwa wa tunguu. Ambapo Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati cochin ina tuguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu.

  • HALI YA HEWA YA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1500 au zaidi. Huitaji mvua kiasi cha mm.1200-1800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigradi 20-25. Hustawi vyema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuwamisha maji.


  • UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 800-1000 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekari moja.
       Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.
       Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 4-8 kwa hekari na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.
     Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, na kawaida ni mara nne (4) wakati huo katika palizi ya tatu na ya nne hushauliwa kupandishia udongo kwa kila china la mmea ili kuupa mmea nafasi ya kutoa tunguu kubwa na nene
       Pia dawa ya kuuwa wadudu kama simazine hutumika.

  • MAGONJWA NA WADUDU
  • Madoa ya majani yanayosababishwa na
viini vya magonjwa viitwavyo
Colletotrichum zingiberisna Phyllosticta
zingiberi.
  • Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na
viini viitwavyo Pithium spp.
  • Mizizi fundo; inasababishwa na viini viitwavyomeloidegyne spp.

  • UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana
kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 8-12 cha
tangawizi mbichi huweza kupatikana.

  • USINDIKAJI
  • Ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16%-18%.

  • SOKO LA TANGAWIZI
Soko la Tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, Hapa nchini huuzwa kwa bei ya Tshs. 2000-4000/= `kutegemea na msimu.

ZIFAHAMU MBEGU MPYA BORA ZA MAHINDI.

Kituo: Selian Agricultural Research Institute - Arusha

Mbegu: Selian H215
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika mwinuko wa mita 800 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kati ya siku 105 hadi 148.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5 kwa hekta.
  • Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) hususan katika maeneo ya kanda ya kaskazini. 
Kituo: Kituo Cha Utafiti Ilonga – Kilosa Morogoro
Mbegu: 1. WE4106
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 106.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame.

2. WE4102
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 105.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.7 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame.

3. WE4110
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 101 hadi 111.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu
  • wa majani (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability)
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.6 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame. 

4. WE4114
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 102.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.9 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame.

4. WE4115
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 112.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.4 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame.

5. WE4112
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 103.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), Ukungu kijivu wa mahindi (grey Leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability)
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.5 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame. 

Kituo: Kituo Cha Utafiti Tumbi - Kibaha
Mbegu: 1. T104
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)
  • Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,500.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 128.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.5 kwa hekta.

2. T105
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)
  • Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1500.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 103 hadi 129.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.4 kwa hekta.

Kituo: Aminata Quality Seeds & Consultancy Ltd - Tanga
Mbegu: 1. NATA H401
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 400 hadi 1,500.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 120 hadi 130.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7 kwa hekta.
  • Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot), baka jani (leaf blight) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).

2. NATA K 8
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 0 hadi 1,600.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 110 hadi 120.
  • Inastahimili magonjwa ya bakajani wa mahindi (grey leaf spot), milia (maize streak virus) na ‘Turcicum blight’.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.9

Kituo: Krishna Seed Company Ltd – Babati Manyara
Mbegu: 1. Krishna Hybrid-1
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa muda wa siku 128.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.9 kwa hekta.
  • Inastahimili magonjwa ya majani wa ukungu kijivu wa mahindi (grey leaf spot) milia ya mahindi (maize streak virus).

2. Krishna Hybrid-2
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa muda wa siku 134.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7.6 kwa hekta.
  • Inastahimili magonjwa ya ukungu kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).

Kituo: Meru Agro- Tours & Consultancy Co. Ltd – Arusha
Mbegu: 1. MERU LISHE 503
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
  • Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.
  • Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa mapema kwa wastani wa siku 99.
  • Ina stahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi(grey leaf spot)na milia ya mahindi ( maize streak virus).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.3 kwa hekta.
  • Inakoboleka kirahisi.

2. MERU LISHE 511
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
  • Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.
  • Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa muda wa wastani wa siku 98.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.2 kwa hekta.
  • Inakoboleka kirahisi. 
Kituo: Iffa Seed Company Ltd - Arusha
Mbegu: 1. Kaspidi hybrid
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Hustawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa muda wa siku 150 hadi siku 155.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.1 kwa hekta.
  • Inastahimili magonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus). 

2. Kisongo hybrid
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Hustawi katika ukanda wa mwinuko wa mita 600 had 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa katika siku 138.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.
  • Inastahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus). 

HABARI NJEMA KWA WAKULIMA, NAFAKA BADO YASHIKILIA PALE PALE.

Hali ya soko masokoni katika masoko makuu ya mikoani hapa nchi bado iko vizuri, ambapo mazao hayajapanda wala kushuka kulinganisha na wiki i...