Monday, July 3, 2017

ZIFAHAMU MBEGU MPYA BORA ZA MAHINDI.

Kituo: Selian Agricultural Research Institute - Arusha

Mbegu: Selian H215
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika mwinuko wa mita 800 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kati ya siku 105 hadi 148.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5 kwa hekta.
  • Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) hususan katika maeneo ya kanda ya kaskazini. 
Kituo: Kituo Cha Utafiti Ilonga – Kilosa Morogoro
Mbegu: 1. WE4106
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 106.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame.

2. WE4102
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 105.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.7 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame.

3. WE4110
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 101 hadi 111.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu
  • wa majani (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability)
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.6 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame. 

4. WE4114
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 102.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.9 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame.

4. WE4115
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 112.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.4 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame.

5. WE4112
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 103.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), Ukungu kijivu wa mahindi (grey Leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability)
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.5 kwa hekta.
  • Inastahimili ukame. 

Kituo: Kituo Cha Utafiti Tumbi - Kibaha
Mbegu: 1. T104
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)
  • Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,500.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 128.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.5 kwa hekta.

2. T105
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)
  • Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1500.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 103 hadi 129.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.4 kwa hekta.

Kituo: Aminata Quality Seeds & Consultancy Ltd - Tanga
Mbegu: 1. NATA H401
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 400 hadi 1,500.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 120 hadi 130.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7 kwa hekta.
  • Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot), baka jani (leaf blight) na kutu ya majani (leaf rust).
  • Inakoboleka vizuri (good poundability).

2. NATA K 8
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
  • Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 0 hadi 1,600.
  • Inakomaa kwa wastani wa siku 110 hadi 120.
  • Inastahimili magonjwa ya bakajani wa mahindi (grey leaf spot), milia (maize streak virus) na ‘Turcicum blight’.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.9

Kituo: Krishna Seed Company Ltd – Babati Manyara
Mbegu: 1. Krishna Hybrid-1
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa muda wa siku 128.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.9 kwa hekta.
  • Inastahimili magonjwa ya majani wa ukungu kijivu wa mahindi (grey leaf spot) milia ya mahindi (maize streak virus).

2. Krishna Hybrid-2
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa muda wa siku 134.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7.6 kwa hekta.
  • Inastahimili magonjwa ya ukungu kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).

Kituo: Meru Agro- Tours & Consultancy Co. Ltd – Arusha
Mbegu: 1. MERU LISHE 503
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
  • Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.
  • Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa mapema kwa wastani wa siku 99.
  • Ina stahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi(grey leaf spot)na milia ya mahindi ( maize streak virus).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.3 kwa hekta.
  • Inakoboleka kirahisi.

2. MERU LISHE 511
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
  • Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.
  • Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa muda wa wastani wa siku 98.
  • Ina ukinzani wa magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.2 kwa hekta.
  • Inakoboleka kirahisi. 
Kituo: Iffa Seed Company Ltd - Arusha
Mbegu: 1. Kaspidi hybrid
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Hustawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa kwa muda wa siku 150 hadi siku 155.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.1 kwa hekta.
  • Inastahimili magonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus). 

2. Kisongo hybrid
Sifa za mbegu
  • Aina hii ni mahindi chotara.
  • Hustawi katika ukanda wa mwinuko wa mita 600 had 1,200 kutoka usawa wa bahari.
  • Inakomaa katika siku 138.
  • Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.
  • Inastahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus). 

No comments:

Post a Comment

HABARI NJEMA KWA WAKULIMA, NAFAKA BADO YASHIKILIA PALE PALE.

Hali ya soko masokoni katika masoko makuu ya mikoani hapa nchi bado iko vizuri, ambapo mazao hayajapanda wala kushuka kulinganisha na wiki i...