Monday, July 3, 2017

KILIMO CHA TANGAWIZI

  • UTANGULIZI
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Ambao huonekana kama mizizi ya mmea. Mmea huu kitaalamu huitwa zingiber officinale.
       Asili ya mmea huu sehemu za kitropiki za bara la Asia hasa nchi za china za india. Zao hili huzalishwa kwa wingi nchini Jamaica.
    Hapa nchini zao hili huweza kustawi katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Ruvuma, kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.



  • MATUMIZI
Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na changamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, n.k
   Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k.

      
  • TABIA YA MMEA
Kama nilivyodokeza hapo juu, mmea huu huvunwa kama Tunguu hivyo basi; hutambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi.
       Ingawa hadi sasa kitaalamu haijasibitishwa kuwa ni aina gani ya tangawizi hulimwa hapa Madaba. Wengine husema ni white Africa (Jamaica)na wengine husema cochin (flint). Ambazo ndio maarufu hapa nchini Tanzania.
       Kikubwa sio aina ya mmea bali uwezekano wa kustawi na kutoa matunda mazuri, aina hizi hutofautiana tu katika majani na ukubwa wa tunguu. Ambapo Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati cochin ina tuguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu.

  • HALI YA HEWA YA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1500 au zaidi. Huitaji mvua kiasi cha mm.1200-1800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigradi 20-25. Hustawi vyema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuwamisha maji.


  • UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 800-1000 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekari moja.
       Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.
       Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 4-8 kwa hekari na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.
     Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, na kawaida ni mara nne (4) wakati huo katika palizi ya tatu na ya nne hushauliwa kupandishia udongo kwa kila china la mmea ili kuupa mmea nafasi ya kutoa tunguu kubwa na nene
       Pia dawa ya kuuwa wadudu kama simazine hutumika.

  • MAGONJWA NA WADUDU
  • Madoa ya majani yanayosababishwa na
viini vya magonjwa viitwavyo
Colletotrichum zingiberisna Phyllosticta
zingiberi.
  • Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na
viini viitwavyo Pithium spp.
  • Mizizi fundo; inasababishwa na viini viitwavyomeloidegyne spp.

  • UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana
kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 8-12 cha
tangawizi mbichi huweza kupatikana.

  • USINDIKAJI
  • Ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16%-18%.

  • SOKO LA TANGAWIZI
Soko la Tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, Hapa nchini huuzwa kwa bei ya Tshs. 2000-4000/= `kutegemea na msimu.

No comments:

Post a Comment

HABARI NJEMA KWA WAKULIMA, NAFAKA BADO YASHIKILIA PALE PALE.

Hali ya soko masokoni katika masoko makuu ya mikoani hapa nchi bado iko vizuri, ambapo mazao hayajapanda wala kushuka kulinganisha na wiki i...